MJUE BIBI TITI MWANAMKE SHUJAA NA HODARI MWENYE HISTORIA YA KPKEE TANZANIA
+255 🇹🇿🇹🇿🇹🇿 BIBI TITI MOHAMED: MWANAMAMA SHUPAVU NA MPIGANIA UHURU HODARI ALIYETINGISHA NA KUHESHIMIKA AFRIKA MASHARIKI NZIMA!!! 1. Usuli: 1.1 TITI Kuzaliwa: TITI MOHAMED SALUM MANDWAGA alizaliwa mwezi Juni 1926 jijini Dsm. 1.2 Wazazi Wa TITI: Baba yake aliitwa Bw. MOHAMED BIN SALIM na mama yake aliitwa Bi. HADIJA BINTI SALIM. Wazazi hawa walitokea Rufiji. Baba yake alikuwa mfanyabiashara ya mbuzi na ng'ombe na mama yake alikuwa mkulima. 2. Elimu: 2.1 Baba Agoma TITI Asisome: Baba yake alikataa katukatu kwamba TITI asisome shule kwa hofu angekuwa kafiri. 2.2 Mama Ampeleka TITI Shule: Baba yake alifariki TITI akiwa na miaka 9 tu. Mamaye akatumia fursa hiyo kumpeleka TITI Shule ya Wasichana Uhuru ambako alisoma hadi darasa la 4. 3. TITI Aolewa na MHENGA akiwa na miaka 14 tu: TITI aliolewa na mwanaume mzee ambaye angeweza hata kuwa baba yake wakati yeye akiwa binti wa miaka 14 tu. 4. TITI Ajifungua M...