KUELEKEA MTIHANI WA TAIFA MWEZI MEI, WANAFUNZI 1003 KIDATO CHA SITA SIMIYU WAPIGA KAMBI YA KITAALUMA
Na Stella Kalinga Simiyu Takribani wanafunzi 1003 wa Kidato cha sita kutoka shule za Sekondri 11 zenye kidato cha tano na sita Mkoani Simiyu wamepiga kambi katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na Shule ya Sekondari Binza, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mtihani wa Taifa ambao unatarajia kufanyika mapema mwezi Mei mwaka huu. Akifungua kambi hiyo leo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wilayani Maswa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amesema ili mkoa huo uweze kushindana na kufanya mageuzi katika Uchumi ni lazima kuwekeza katika elimu. “Kama wanafunzi wetu wanakaa makambi ya michezo ngazi ya kata, wilaya, mkoa na Taifa kwa nini wanafunzi hao hao wasikae kambi kwa ajili ya maendeleo ya taaluma; tukitaka kufanya mageuzi ya Mkoa huu ni lazima tuweke nguvu kwenye elimu, maeneo yenye uchumi mzuri wamewekeza sana kwenye elimu” alisema Mtaka. Aidha, Mtaka awataka wanafunzi wote wa kidato cha sita kuwasikiliza walimu watakaokuwa wakiwafu...