ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MADINI MHESHIMIWA NYONGO MKOANI IRINGA....

Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo leo Januari 14, ameanza rasmi ziara ya kukagua shughuli za uchimbaji madini katika Mkoa wa Iringa. Akiwa Mkoani humo, Naibu Waziri ametembelea na kukagua mgodi wa Ulata katika kijiji cha Ulata, Kata ya Uwasa Wilaya ya Iringa. Mbali ya kutembelea mgodi huo, pia amesikiliza kero za wachimbaji mgodi hapo akilenga kutatua mgogoro baina ya mmiliki wa mgodi huo na wachimbaji wadogo. Aidha, mbali ya kutatua mgogoro huo, amepata fursa ya kuzungumza na wachimbaji hao ambao wametoa kero zao. Taarifa zaidi kuhusu alichokizungumza Naibu Waziri itawaijia. Tangaza Nasi UVCCM Maswa Bureee kupitia Blog yetu Tushirikishe 0758092500