Posts

Showing posts from January, 2019

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MADINI MHESHIMIWA NYONGO MKOANI IRINGA....

Image
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo leo Januari 14, ameanza rasmi ziara ya kukagua shughuli za uchimbaji madini katika Mkoa wa Iringa. Akiwa Mkoani humo, Naibu Waziri ametembelea  na kukagua mgodi wa Ulata katika kijiji cha Ulata, Kata ya Uwasa Wilaya ya Iringa. Mbali ya kutembelea mgodi huo, pia amesikiliza kero za wachimbaji mgodi hapo akilenga kutatua mgogoro  baina ya mmiliki wa mgodi huo na wachimbaji wadogo. Aidha, mbali ya kutatua mgogoro huo, amepata fursa ya kuzungumza na wachimbaji hao  ambao wametoa kero zao. Taarifa zaidi kuhusu alichokizungumza Naibu Waziri itawaijia. Tangaza Nasi UVCCM Maswa  Bureee kupitia Blog   yetu Tushirikishe 0758092500

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM MASWA MKOANI SIMIYU YALETA NEEMA UKAMILISHWAJI WA JENGO LA KITEGA UCHUMI LA CCM. NYONGO ASHITUKIZA HARAMBEE

Image
Ziara ya katibu mkuu wa  chama cha mapinduzi CCM Taifa  Dr Bashiru Ally mkoani Simiyu Imetamatika katika wilaya ya Maswa ambapo pamoja na Mambo mengine Dr. Bashiru Ally aliweza kusimika Jiwe la  Msingi la  ujenzi wa  jengo la  kitega uchumi. na kuwahutubia mamia ya wanachama wa  CCM waliojitokeza kwa wingi kumraki na kumsikiliza katibu mkuu wa   CCM . katika hatua nyingine Mbunge wa Maswa  Mashariki na Naibu waziri wa  Madini Mheshimiwa Stanslaus . H. Nyongo alipopata wasaa wa  kusalimia aliweza kuhamasisha Harambee ya Papo kwa hapo   ili kukamilisha baazi ya mahitaji ya Jengo hilo Ambapo Mheshimiwa nyongo akiwa kama katibu wa  wabunge wa mkoa wa  simiyu aliwaita wabunge wote   waliokuwepo na akawaomba wamchangie chochote kwaajili ya ukamilishaji waa jengo hilo . Mhe   Nyongo alitoa mifuko 100 ya cement, na wabunge wote   walichangia Bati 150  wak...