ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM MASWA MKOANI SIMIYU YALETA NEEMA UKAMILISHWAJI WA JENGO LA KITEGA UCHUMI LA CCM. NYONGO ASHITUKIZA HARAMBEE
Ziara ya katibu mkuu wa chama cha mapinduzi CCM Taifa Dr Bashiru Ally mkoani Simiyu Imetamatika katika wilaya ya Maswa ambapo pamoja na Mambo mengine Dr. Bashiru Ally aliweza kusimika Jiwe la Msingi la ujenzi wa jengo la kitega uchumi. na kuwahutubia mamia ya wanachama wa CCM waliojitokeza kwa wingi kumraki na kumsikiliza katibu mkuu wa CCM.
katika hatua nyingine Mbunge wa Maswa Mashariki na Naibu waziri wa Madini Mheshimiwa Stanslaus. H. Nyongo alipopata wasaa wa kusalimia aliweza kuhamasisha Harambee ya Papo kwa hapo ili kukamilisha baazi ya mahitaji ya Jengo hilo Ambapo Mheshimiwa nyongo akiwa kama katibu wa wabunge wa mkoa wa simiyu aliwaita wabunge wote waliokuwepo na akawaomba wamchangie chochote kwaajili ya ukamilishaji waa jengo hilo.
Mhe Nyongo alitoa mifuko 100 ya cement, na
wabunge wote walichangia Bati 150 wakiongozwa na MTEMI CHENGE mbunge wa bariadi.
Mheshimiwa jambo alitoa million mbili
Mheshimiwa Ester Midimu (MB) viti malaum kwa niaba wa Madiwani wa viti malum alitoa million Moja,
Mheshimiwa Mkuu wa mkoa was Simiyu Rc, Mtaka Fedha laki tano.
na kamati ya siasa mkoa wa simiyu ikatoa mifuko hamsini ya Cement
Ambapo katibu mkuu akahitimisha harambee kwa kuchangia kiasi cha million moja
kwa ziara hii ya katibu mkuu pamoja na mambo yote chama cha mapinduzi wilaya ya Maswa tumepata jumla ya kiasi cha fedha million NNE na laki tano, mifuko ya cement 150 na Bati 150.
Kwa niaba ya chama cha mapinduzi UVCCM Maswa tunamshukuru Dr. Bashiru Ally katibu mkuu was CCM na pia wabunge na viongozi wote mlioweza kuchangia CHAMA ili kupiga hatua ujenzi wa jengo la kitega uchumi aiza pasipo kutarajia kuwa itafanyika harambee chama cha Mapinduzi tuna mshukuru Mbunge wa Maswa mashariki Na naibu waziri wa madini Mhe Nyongo. kwa kushitukiza harambeee.
imetolewa na UVCCM Maswa
0758092500
Lea Komanya hakuwepo kama mwandishi alivyoandika, Bali aliyechangia kwa niaba ya madiwani ni Ester Midimu mbunge wa viti maalumu....pamoja na mambo mengine pia alizungumzia uhamisho wa makatibu wa wilaya kuwa wanafanya vizuri, amewahamisha ili wakafanye kazi.
ReplyDelete