Posts

Showing posts from May, 2022

Mti mwema. Wenye maajabu.

Basi kukapambazuka siku yenyewe na mvua ilikuwa Bado inanyesha hata hivyo ilikuwa mvua ya wastani japokuwa watu hawakukata tamaa kuelekea kunako shughuli zao za Kila siku. Wakati tunatoka Ndani ya nyumba nje yake kulikuwa na mti aina ya mkwaju nikashangaa kuona matunda yake yakiwa yamekomaa yamewiva vizuri lakini matunda menyewe yapo utupu yaani yamemenywa ingali Bado yapo mtini na Kwa sababu ya mvua na unyevu ukwaju ule ulikuwa ukinata, Cha ajabu nilipotaka kuchuma walau tunda mojawapo ndipo macho yangu yakakutana uso Kwa uso na joka kubwa aina ya chatu, Ambapo kwenye huo mti lipo pango joka Hilo linaishi. Joka Hilo kubwa likaanza kutuvizia kuja upande tuliokuwa  kutaka kutumeza hata hivyo mawe yaliyokuwa chini, ng'hambo kidogo tuliyatumia kuliponda na baadae likawa limerudi Ndani ya pango lake kwenye utando wa mti huo wa mkwaju. Nikamwambia rafiki yangu mti huu hupondwa si Kwa sababu ya matunda Ila hupondwa Kwa sababu joka hili  juu ya mti, katikati linaziba au kuzuia ridhiki ya ...