Mti mwema. Wenye maajabu.
Basi kukapambazuka siku yenyewe na mvua ilikuwa Bado inanyesha hata hivyo ilikuwa mvua ya wastani japokuwa watu hawakukata tamaa kuelekea kunako shughuli zao za Kila siku.
Wakati tunatoka Ndani ya nyumba nje yake kulikuwa na mti aina ya mkwaju nikashangaa kuona matunda yake yakiwa yamekomaa yamewiva vizuri lakini matunda menyewe yapo utupu yaani yamemenywa ingali Bado yapo mtini na Kwa sababu ya mvua na unyevu ukwaju ule ulikuwa ukinata, Cha ajabu nilipotaka kuchuma walau tunda mojawapo ndipo macho yangu yakakutana uso Kwa uso na joka kubwa aina ya chatu, Ambapo kwenye huo mti lipo pango joka Hilo linaishi. Joka Hilo kubwa likaanza kutuvizia kuja upande tuliokuwa kutaka kutumeza hata hivyo mawe yaliyokuwa chini, ng'hambo kidogo tuliyatumia kuliponda na baadae likawa limerudi Ndani ya pango lake kwenye utando wa mti huo wa mkwaju.
Nikamwambia rafiki yangu mti huu hupondwa si Kwa sababu ya matunda Ila hupondwa Kwa sababu joka hili juu ya mti, katikati linaziba au kuzuia ridhiki ya wengi Kwa Maana familia au watu wanaotaka kuchuma matunda haya hivyo tuondoke, katika harakati za kuondoka kwenye ngome hiyo yenye uzuio wa minyaa na miba ghafra joka Hilo likaanza kutokea Kwa haraka zaidi kuelekea ghetini ulipo mlango wa kutokea mwenzangu akaniambia tun'goe sehemu yoyote tutoke Maana joka limezuia ghetini na hatuna Cha kujihami nalo, tukafanikiwa Kutoka Kwa kupitia pale tulipobomoa uzio hata hivyo joka lile lilitufuata Kwa nje na kutuface hukohuko nje kwakuwa hatukuwa na silaha yoyote basi kwa akikiri ya Muda huo nilichokifanya ni kuchukua mchanga nikajaribu kulimwagia usoni ili lisione lakini ghafla nikazinduka usingizini.
Hata hivyo Kuna Cha kujifunza zaidi juu ya Ndoto kama hizi.
- Joka Ndani ya uzio wa nyumba juu ya mti mwema
- Mti wenye matunda tena yanavutia Kwa kuliwa lakini lipo joka juu yake.
- Mti umepondwa mawe au joka hupondwa mawe?
Comments
Post a Comment