KUTOKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MWALIMU JULIUS NYERERE DAR.

YALIYOJIRI WAKATI WA MAPOKEZI YA NDEGE MPYA YA AIRBUS 220-300 KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE LEO TAREHE 23 DESEMBA, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli #Nawapongeza watanzania kwa kuamua kulipa kodi, tunafanya haya kwa sababu ya kulipa kodi, hongereni sana Watanzania. #Watanzania nawasisitiza tuwe wazalendo, hii ni kwa faida ya taifa letu. #Uchumi wa nchi yetu unaenda vizuri, tutunze amani yetu, tunarasilimali nyingi, Tanzania ni tajiri. #Pamoja na kuleta ndege mpya tunafufua karakana yetu kubwa ya matengenezo ya ndege iliyopo Kilimanjaro. #Tuliahidi kuimarisha huduma za usafiri, na katika miaka hii mitatu tumetekeleza ahadi hii kwa vitendo ikiwa ni kwa kufanya mambo makubwa ardhini, angani na hata majini. #Tunafanya upanuzi na ukarabati wa viwanja vya ndege 11 nchini, lengo ni kuendelea kuboresha sekta ya usafiri wa anga. #Watendaji wakuu wa Serikali waliolipiwa tiketi za ndege za ATCL na hawakusafiri warudishe fedh...