KUTOKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MWALIMU JULIUS NYERERE DAR.
YALIYOJIRI WAKATI WA MAPOKEZI YA NDEGE MPYA YA AIRBUS 220-300 KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE LEO TAREHE 23 DESEMBA, 2018
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
#Nawapongeza watanzania kwa kuamua kulipa kodi, tunafanya haya kwa sababu ya kulipa kodi, hongereni sana Watanzania.
#Watanzania nawasisitiza tuwe wazalendo, hii ni kwa faida ya taifa letu.
#Uchumi wa nchi yetu unaenda vizuri, tutunze amani yetu, tunarasilimali nyingi, Tanzania ni tajiri.
#Pamoja na kuleta ndege mpya tunafufua karakana yetu kubwa ya matengenezo ya ndege iliyopo Kilimanjaro.
#Tuliahidi kuimarisha huduma za usafiri, na katika miaka hii mitatu tumetekeleza ahadi hii kwa vitendo ikiwa ni kwa kufanya mambo makubwa ardhini, angani na hata majini.
#Tunafanya upanuzi na ukarabati wa viwanja vya ndege 11 nchini, lengo ni kuendelea kuboresha sekta ya usafiri wa anga.
#Watendaji wakuu wa Serikali waliolipiwa tiketi za ndege za ATCL na hawakusafiri warudishe fedha wenyewe tunataka thamani ya fedha zetu.
#Naamini pia wafanyakazi wa Air Tanzania mtaendelea kuhakikisha mnazalisha faida na kutoa huduma bora maana nimeanza kuona baadhi ya malalamiko.
*Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe*
#Tutafanya kila jitihada za kuhakikisha tunaendelea kuliboresha Shirika letu la ndege.
#Tumeweka mipango ya kufufua karakana yetu ya matengenezo ya ndege iliyopo Kilimanjaro, ndege zetu zitakarabatiwa hapahapa.
*Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Balozi John Kijazi*
#Ndege hii ni ya tano kuwasili nchini katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Magufuli na Tanzania ni ya kwanza Afrika kununua ndege hii.
#Mwezi January tunategemea kupokea ndege nyingine kama hii.
*Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuhiro*
#Leo tunapokea ndege moja kati ya mbili ikiwa ni sehemu ya mpango wa ufufuaji wa Shirika letu la ndege.
#Ndege hizi ni mpya kabisa na za kisasa , Tanzania ndio nchi ya kwanza barani Afrika kununua ndege hizi na zina uwezo wa kubeba abiria 132.
#Ndege hizi zinauwezo wa kuruka moja kwa moja bila kusimama kwa masaa sita na nusu.
#Idadi ya abiria wanaotumia Shirika leo wameongezeka kutoka 5600 hadi kufikia abiria 34,000 kwa mwezi.
*Mkuu wa Mkoa wa Dar wa Dar es Salaam Mhe. Paul Makonda*
#Maendeleo haya yote ni kwasababu watanzania tumeamua kuungana na kulipa kodi, tuendelee kufanya hivi kwa ustawi wa nchi yetu.
Imetolewa na Idara ya Habari- MAELEZO
UVCCM MASWA NGUVU MOJA
Comments
Post a Comment