DAKIKA 45 ZA KIPINDI CHA KWANZA KWANU WATEULE

Ndugu watanzania wenzangu , mabibi na mabwana vijana kwa wazee, nianze kwa kumshukuru Mungu kwa uzima na afya njema kwetu sote lakini nitoe pole kwa wale wote ambao hali zenu sio nzuri kiafya pamoja na mambo mengine, hata hivyo kila lililo kheri nawatakieni. Nianze kwa kumpongeza Dr John Pombe Magufuli Rais wa awamu ya tano wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa mara nyingine kwa kuaminiwa na watanzania wote kuendelea kuwaongoza kwa ushindi wa kishindo wa zaidi ya asilimia 81, wakiwa pamoja na mwana mama hodari kabisa Samia Hassan katika uchaguzi mkuu wa october 2020. lakini kwa kipekee nikipongeze chama cha mapinduzi CCM chini ya uongozi wa dr John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuaminika na Umma wa Tanzania hata hivyo pongezi ziende kwao viongozi wa CCM wa ngazi zote kwa kazi kubwa walizofanya katika kuhakikisha CCM inaendelea kushinda chaguzi ili kuunda serikali. niishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutekeleza vyema na kishindo ilani ya uchaguzi ya mwaka 20...