DAKIKA 45 ZA KIPINDI CHA KWANZA KWANU WATEULE
Ndugu watanzania wenzangu , mabibi na mabwana vijana kwa wazee, nianze kwa kumshukuru Mungu kwa uzima na afya njema kwetu sote lakini nitoe pole kwa wale wote ambao hali zenu sio nzuri kiafya pamoja na mambo mengine, hata hivyo kila lililo kheri nawatakieni.
Nianze kwa kumpongeza Dr John Pombe Magufuli Rais wa awamu ya tano wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kwa mara nyingine kwa kuaminiwa na watanzania wote kuendelea kuwaongoza kwa ushindi wa kishindo wa zaidi ya asilimia 81, wakiwa pamoja na mwana mama hodari kabisa Samia Hassan katika uchaguzi mkuu wa october 2020. lakini kwa kipekee nikipongeze chama cha mapinduzi CCM chini ya uongozi wa dr John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuaminika na Umma wa Tanzania hata hivyo pongezi ziende kwao viongozi wa CCM wa ngazi zote kwa kazi kubwa walizofanya katika kuhakikisha CCM inaendelea kushinda chaguzi ili kuunda serikali. niishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutekeleza vyema na kishindo ilani ya uchaguzi ya mwaka 2015-2020 pamoja na mipango ya maendeleo ya muda mfupi na ya muda mrefu iliyoweza kutekelezwa ama kuanza kutekelezwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita ama hakika ni mambo mengi yameweza kufanyika ndio maana hata ushindi wa kishindo nwa CCM si wakutiliwa shaka ni kutokana na utekelezaji mzuri wa ilani ya uchaguzi chini ya Rais Dr Magufuli.
Kwenu wateule, ninawapongeza sana kwa kuaminiwa kwenu na Dr John Joseph Pombe Magufuli kuwa sehemu ya wasaidizi wake katika nafasi zenu mlizo apa mbele yake na mwenyezi Mungu, mmeaminiwa kuwa sehemu ya kutimiza na kutenda kila lililo jema kuhakkisha mosi ile imani ya watanzania kwa serikali yao chini ya Raisi Magufuli inazidi kuimalika kwa maana ya kutenda yaliyoahidiwa na mkalete ubunifu wa namna gani mtatekeleza majukumu yenu ili kuleta ufanisi na huduma iliyo bora kwa watanzania wote. Mmeaminiwa ili msilale mkajisahau na kusahahu nini watanzania wanataka mnapaswa kila mala muwaze na kutenda kwa yale yapaswayo kutenda, mmeaminiwa ili mkawe faraja na sio balaa kwa watanzania, mmeaminiwa ili mkawe neema kwa watanzania, mmeaminiwa ili mkalete mapinduzi makubwa katika sekta zote ili zipige hatua kutoka palae tulipo ili kadri muda unavyokuja tuone mabadiriko na ubora zaidi, hii yote Dr Magufuli amewaamini mkatende pamoja na kuwa sehemu ya washauri wazuri kwake.
niwakumbushe kuwa mkienda kinyume, mkatenda hovyo, mkajisahau kutimiza wajibu wenu na kutenda haki hakika daki 45 za kipindi cha kwanza hamtoboi lakini niwaombee kwa mwneyezi Mungu mkatende kama yalivyo matakwa yake yeye aliyewaamini na matakwa ya watanzania. matakwa ya watanzania ni kuonyeshwa njia ya kupata maendeleo, matakwa ya watanzania ni kupata huduma bora toka kwa serikali yao ambapo na ninyi ni sehemu ya watoaji wa huduma, enendeni mkafanye yaliyomema huku mkikjua wapo watanzania wengi wenye sifa kama zenu au zaidi wamesubiri muanguke ili wakatende yale mambo ya nje ya uwanja. timizeni ili dakika zingine 45 mkaanze ili timu ishinde.
mwisho niwatakie kheri ya kristimasi na mwaka mpya 2021 ukawe mwaka wenye mafanikio na neema kwa serikali mnayoiongoza.
masaga john paul
mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Maswa.
Comments
Post a Comment