Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo leo Januari 14, ameanza rasmi ziara ya kukagua shughuli za uchimbaji madini katika Mkoa wa Iringa. Akiwa Mkoani humo, Naibu Waziri ametembelea na kukagua mgodi wa Ulata katika kijiji cha Ulata, Kata ya Uwasa Wilaya ya Iringa. Mbali ya kutembelea mgodi huo, pia amesikiliza kero za wachimbaji mgodi hapo akilenga kutatua mgogoro baina ya mmiliki wa mgodi huo na wachimbaji wadogo. Aidha, mbali ya kutatua mgogoro huo, amepata fursa ya kuzungumza na wachimbaji hao ambao wametoa kero zao. Taarifa zaidi kuhusu alichokizungumza Naibu Waziri itawaijia. Tangaza Nasi UVCCM Maswa Bureee kupitia Blog yetu Tushirikishe 0758092500
Kwa Hisani ya Mwandishi wa kitabu chake NG'WANAMALUNDI SHUJAA WA WAKISUKUMA ALIYEWATESA WAJERUMANI. Kwa wale waliopata kusoma historia au kusikia hadithi za makabila, hasa ya Wasukuma na Wanyamwezi, hawakukosa kusikia habari ya Ng’wanamalundi. Mtu huyo aliyewahi kuutingisha utawala wa Wajerumani, alizaliwa katika ukoo wa kawaida akiwa mcheza ngoma mashuhuri, mwaka wa kuzaliwa kwake haufahamiki ila alifariki dunia mwaka 1936, akiwa tayari mtu mzima. Watu wengi wamekuwa wakimjadili kwa maoni tofauti, wengine wakimsifu kama shujaa huku wengine wakihusisha uwezo wake na nguvu za giza. Katika makala hii usahihi wa historia yake unaelezwa na mjukuu wake wa pili, Kishosha Sitta (80) mkazi wa Kijiji cha Mwalugulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, anayesimulia alivyomfahamu babu yake huyo. Sitta anaanza kueleza kuwa jina halisi la babu yake halikuwa Ng’wanamalundi bali lilikuwa Igulu Bugomola, ambaye alizaliwa katika Kijiji cha Mwakubunga Nera wilayani Kwimba mkoani Mwa...
Comments
Post a Comment