MAANDAMANO YA CHADEMA KUPITIA KWA MANGE KUNAMBI NI HARAMU WASHIRIKI KUKIONA CHA MTEMAKUNI
Na David Maphone. . NI KWA MUJIBU WA SHERIA NA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA , . . Ni vyema tujaribu kuangalia ni nani anaitisha MAANDAMANO nini kilichoombwa katika hayo MAANDAMANO na nini kilichozuiwa na POLISI katika hayo MAANDAMANO ?. Pia kuangalia sheria inasemaje kuhusu suala hili. NINI HAKI AU STAHILI (ENTITLEMENTS) ZA VYAMA VYA SIASA KUHUSU MAANDAMANO NA MIKUTANO ?: #Sheria za Vyama vya Siasa (Political Parties Act) na za Jeshi la Polisi (Police Force and Auxiliary Services Act) zinatoa stahili ya kufanya mikutano ya hadhara (Public Meetings) na kuongozana (Processions) kwa vyama vya Siasa kwa ajili ya kujitangaza na kutafuta wanachama, Kifungu cha (4) cha sheria ya vyama kinatoa haki hiyo Lakini Kifungu cha (6) cha sheria hiyo hiyo kinatoa Sharti ili chama kifanye maandamano au mkutano wa Hadhara.'' Chama hakitaruhusiwa kufanya mkutano au Maandamano kama kitapokea AMRI PINGAMIZI kutoka Jeshi la POLISI''. #Pia sheria inatoa ...