MAANDAMANO YA CHADEMA KUPITIA KWA MANGE KUNAMBI NI HARAMU WASHIRIKI KUKIONA CHA MTEMAKUNI


Na David Maphone.
.

NI KWA MUJIBU WA SHERIA NA KATIBA YA  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA , .
.
Ni vyema tujaribu kuangalia  ni nani anaitisha MAANDAMANO nini kilichoombwa katika hayo MAANDAMANO na nini  kilichozuiwa na POLISI katika hayo MAANDAMANO ?. Pia kuangalia sheria inasemaje kuhusu suala hili.

NINI  HAKI AU STAHILI (ENTITLEMENTS) ZA VYAMA VYA SIASA KUHUSU  MAANDAMANO NA MIKUTANO ?:

#Sheria za Vyama vya Siasa (Political Parties Act) na za Jeshi la Polisi (Police Force and Auxiliary Services Act) zinatoa stahili ya kufanya mikutano ya hadhara (Public Meetings) na kuongozana (Processions) kwa vyama vya Siasa kwa ajili ya kujitangaza na kutafuta wanachama,  Kifungu cha (4) cha sheria ya vyama kinatoa haki hiyo Lakini Kifungu cha (6) cha sheria hiyo hiyo kinatoa Sharti ili chama kifanye maandamano au mkutano wa Hadhara.'' Chama hakitaruhusiwa kufanya mkutano au Maandamano kama kitapokea AMRI PINGAMIZI kutoka Jeshi la POLISI''.

#Pia sheria inatoa stahili ya kulindwa (Protection) na msaada (Assistance) kutoka kwa vyombo vya usalama ili kufanikisha mikutano kufanyika bila vurugu.

#Kufanya mikutano ya hadhara na kuongozana Chama cha Siasa kinatakiwa kutuma taarifa (Notification) masaa 48 kabla kwa Mkuu wa Polisi wa Eneo (Police officer in charge of the area). Taarifa hiyo inatakiwa itaje jina la chama, muda na eneo, sababu za mkutano kwa ujumla au jambo lingine kama Waziri atakavyoelekeza.Kifungu cha (5) (d)

#Baada ya kutoa taarifa hiyo chama kinaruhusiwa kuendelea na mkutano au kuongozana ISIPOKUWA tu kama kitapokea ZUIO (Stop Order) kutoka kwa Polisi kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 Sura Na 258 Kifungu cha (6). Lazima Zuio liwe kwa maandishi na Polisi lazima itoe sababu ya kuzuia kwa mujibu wa sheria Kifungu (7). (b) au (c) Sheria inasema kwa ufupi sana, Polisi haruhusiwi kutoa zuio isipokuwa tu i) kuna chama kingine kimeomba kufanya mkutano au kuongozana au shughuli nyingine katika eneo hilo hilo na muda uleule ii) mkutano huo unategemewa kutumika kwa sababu ambazo ni kinyume na sheria, uvunjifu wa amani au kuhatarisha usalama wa raia katika eneo hilo.

MABWANA, HAYA NDIO MATAKWA YA SHERIA KWA UFUPI SANA.!!
,
.
Tanzania imepata  MKOSI wa kuwa na Viongozi wa vyama vya siasa WAJANJA WAJANJA hawataki kufuata sheria au wanapozisema au kuzisoma sheria  hawataki kuzieleza kwa UHALISIA wake,Ni kweli kabisa ukisoma Katiba na sheria ya vyama vya siasa MAANDAMANO na MIKUTANO ya HADHARA ni haki kwa vyama vya siasa lakini ili kufanya au kutekeleza haki hiyo sheria imeweka UTARATIBU wa kutekeleza kwanza ndio ufanikishe kufanya Maandamano au Mkutano wa Hadhara. Wanasisa wetu kwenye MASHARTI hawataki kuposoma kabisa wanaishia kwenye HAKI tu,
.

.
Badala ya kupambana na sheria zibadilishwe  ili Kuondoa Suala hili kuwa ni HISANI ya Jeshi la POLISI kuamua ufanye au usifanye MAANDAMANO au MIKUTANO  viongozi wa vyama wanatumia muda mwingi kusema UONGO kwamba POLISI wanavunja SHERIA wakati sio KWELI  kabisa . Vifungu hapo juu wanavijua na wanavisoma, KIFUPI Jeshi la POLISII ndio mwenye uamuzi wa chama kufanya mkutano au maandamani kwa mujibu wa sheria tuwe WAKWELI WANASIASA tena sababu za POLISI ziwe za msingi au sio za msingi kwa sababu zinatoka kwao wenyewe,

#NaBado David Maphonekatika ubora wake miaka 800.

Comments

Popular posts from this blog

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MADINI MHESHIMIWA NYONGO MKOANI IRINGA....

MWANAMALUNDI, MSUKUMA ALIYEMSHINDA MKOLONI