TUUNGE MKONO JUHUDI ZA VIONGOZI WETU TUIJENGE MASWA YETU

      MASWA YETU
         Anaandika mothes mbembela

Ndugu wapenzi wasomaji wa Makala zangu Napenda kuwaalika tena katika uchambuzi wa makala zangu ambazo mara nyingi zimekuwa zikiegemea katika kujadili masuala mbalimbali kutoka katika wilaya yangu ya Maswa mkoani Simiyu.
Leo katika makala hii ningependa kujikita zaidi katika kutabainisha mambo mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na kisiasa ambayo kwa kiasi kikubwa yanafanya MASWA YETU ionekane angavu Daima. Katika wilaya yetu Maswa Juhudi mbalimbali zimeweza kufanywa na viongozi kwa kushirikiana na wananchi wao kuhakikisha kuwa wilaya yetu haipo mbali ktk kilele cha maendeleo, kwa ufupi tu niweze kuorodhesha mambo na assets mbalimbali ambazo kwa Hakika Maswa Tunajivunia.
1. Tuna Hospitali kubwa ya wilaya ambayo imekuwa ikihudumia maelfu ya wagonjwa kutoka sehem mbalimbali za nchi yetu tena kwa kiwango cha juu kabisa (Science and Technology) Hongera ya pekee imfikie Dokta Shija kwa Uchapakazi na uhodari ktk kazi.

2. Maswa imejenga shule nyingi za msingi na sekondari kila kata kuhakikisha Sera ya kupata elimu kwa kila mtoto Inawezekana mfano wa shule hzo ni Binza Primary & secondary with Advanced level, Maswa Girls High School, Sola primary, Malita, Dodoma, Buchambi, Nyalikungu, Nyanguganwa, Buyubi, Zanzui, Nhami, Sayusayu, Kinamwigulu n.k

3. Maswa tuna bwawa kubwa la Maji ambalo limekuwa likihudumia wilaya nzima ktk viunga vyote kwa maji safi na salama kutoka Bwawa la Zanzui kilometa kadhaa kutoka ktk mji wa Maswa, Licha ya bwawa hilo kutoa huduma ya Maji wakazi wa kijiji hicho hulitumia kwa uvuvi ambao umekuwa ukiongeza kipato cha taifa na maendeleo ktk jamii husika Hongereni Maswa.

4. Wilaya yetu ina maeneo makubwa ya rasilimali ya misitu ambayo kwa kiasi kikubwa imekuwa hifadhi ya baadhi ya wanyama na pia ni kama chanzo cha mvua ambayo husaidia kuondoa ujangwa na ukame ambao umekuwa kama tatizo katika wilaya yetu. Mfano mzuri ni maliasili ya sola n.k

5. Kilimo na Ufugaji ni jadi yetu sisi wakazi wa maswa na wasukuma kwa ujumla, ktk wilaya yetu wakulima wamijidhatiti kulikomboa taifa  kupitia kilimo cha mkono ambacho kimekuwa kama uti wa mgongo wa taifa letu tangu mwaka 1961 chini ya Sera ya kilimo cha kufa na kupona ya Mwl NYERERE. Hivyo wakazi hawa wamekuwa wakilima mazao ya biashara kama Pamba, Dengu, Mpunga, Miwa, pamoja na mazao ya chakula kama mahindi. Mfano mzuri ni familia ya Mzee SOTERY KANZA MADAHA, FAUSTINE MBUSHI Na familia ya marehemu FABIAN CHAI ni jukumu la serikali kutoa mchango wake kwa wakulima hawa ili kufanisi uchumi wa Taifa letu.

6. Ujenzi wa barabara kuu kwa kiwango cha lami unaoendelea kwa kasi sana kutoka Mwigumbi kwenda Bariadi unaongeza kasi na chachu ya maendeleo katika wilaya yetu chini ya Rais John Pombe Magufuli.

7. Maswa imefanikiwa kuwa na kiwanda cha Chaki ambacho kipo mjini mkabala na hospitali kubwa ya wilaya ambapo kiwanda hicho kimekuwa kikitengeneza chaki ktk kiwango na ubora wa hali ya juu (Quality and Quantity) Pia kupitia kiwanda hicho kimeweza kupanua fulsa za ajira kwa vijana.

8. Wilaya ya Maswa imefanikiwa kuwa na kituo bora cha Matangazo (Radio) ambacho kimekuwa kikisikika sehem mbalimbali za Tanzania kikijulikana kama REDIO SIBUKA FM.

9. Biashara na Ujasiriamali ni moja ya kitengo ambacho hatuwezi kukitupa katika mji wetu kwani tunao wajasiriamali na vikundi mbalimbali vyenye dhamira ya dhati ya ukombozi haswa kwa akina mama, pia tunao wafanya biashara wakubwa wanaotoa huduma mbalimbali ktk jamii yetu pamoja na kupanua masoko mbalimbali.

10. Maswa imejaliwa kuwa na mito mikubwa na midogo ambayo imekuwa ikitiririsha maji yake katika misimu yote ya kiangazi na masika ambayo kupitia vyanzo hivyo vya maji wakazi wake hupata fursa za kuanzisha miradi mbalimbali kama kilimo cha umwagiliaji haswa kwa mto SIMIYU pia mifugo hupata maji safi na salama kwa malisho yao.

Hivyo Basi hayo ni baadhi tu ya mambo ambayo maswa tunajivunia ni jukumu la serikali kuona ni jinsi gani Wilaya hii imedhamiria kupita ktk mkufu wa mapinduzi ya kimaendeleo pia itoe mchango kwa ajiri ya kufanisi masuala yote tajwa hapo juu.
Tusipochukua Hatua Mapema Tutachelewa Na Tukichelewa Hatutafika
UZALENDO KWANZA, MASWA NI YETU, TUIJENGE PAMOJA.

Comments

  1. Maswa ni wilaya kubwa sana,lakini hadi leo ina shule mbili tu za advance ni aibu,ina vituo vitatu tu vya Afya ni aibu kubwa,mpaka leo maswa kuna vijiji havina zahanati,barabara vijijini ni shida,sekondari hazina hostel.Hivyo basi MASWA tunarudia hatusongi mbele

    ReplyDelete
  2. maendeleo ni mchakato na ni hatua hata hizo sekondary hazikuwepo hapo awali

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MADINI MHESHIMIWA NYONGO MKOANI IRINGA....

MWANAMALUNDI, MSUKUMA ALIYEMSHINDA MKOLONI