Mwaka mmoja wa Mwenyekiti wa UVCCM (w) maswa.

Ni mwaka mmoja sasa tangu uchaguzi wa Chama NA jumuia Ngazi ya wilaya NA kukamilika kwa safu ya uongozi kwa ngazi ya wilaya NA jumuia zake, Naam nilipata dhamana kubwa ya kuiongoza jumuia ya Vijana wenzangu kwa ngazi ya wilaya nikipata heshima ya kuwa Mwenyekiti uchaguzi uliokuwa wa Uhuru NA haki.
Jumuia ya Vijana ni jumuia ambayo imebeba Leo yao NA kesho yao kwa vijana tunajitahidi sana kuyasemea mahitaji yao. NA pia kuzitatua changamoto zao kazaa, ikiwemo Ajira, Elimu, ujasiriamali, Mikopo vyuo na vyuo vikuu uwezeshwaji wa vijana hasa kupitia miradi yao kama MBOs, NGs, na hasa uwezeshwaji wao wa mikopo nafuu Kutoka halmashauri yetu ya Maswa. Lakini katika kipindi hiki cha mwaka mmoja tumeendelea kuwafikia vijana wenzetu hasa kupitia ziara ambapo tunapata nafasi ya kuwasikiliza kuwashauri na kuwajengea uwezo na kuwapa Hamasa ya kuyakabiri MAISHA ndani ya Chama na MAISHA ya kawaida nje ya Chama ( we are  empowering them and sensitizes, for their self awareness) ili kupata vijana supa na wanaojitambua kwa maslahi yao na Chama chetu cha mapinduzi.
Bado sisi kama jumuia tunaamini michezo ni sehemu mhumu inayowaunganisha vijana na kuwaweka pamoja, tumeendelea kuwatafutia fursa ya wao kupata vifaa vya michezo ili waendelee kukutana na kubadikishana mawazo(sharing their different ideas ana skill with experience) ili waendelee kuwapo pamoja NA #UMOJANDIO USHINDI.

Nitumie nafasi hii kuwashukuru sana sana kwanza halmashauri wa wilaya ya Maswa chini ya Mkuu wetu wa wilaya Doctor self Shekllage, na mkrugenzi wetu wa wilaya ya Maswa kwa maana wao ndio watendaji wakuu na watekelzaji wakuu wa ilani ya Chama cha mapinduzi kwa ngazi ya wilaya  kwani  Vijana wa Maswa pamoja na changamoto zao wamekuwa wakitengewa fedha zao na halmashauri kwa muda. Na kwamba ofisi ya Mkuu wa wilya na Mkurugenzi wamekuwa wakiwahamasisha vijana kuunda vikundi ili wapewe mikopo jambo ambalo kila mwaka vikundi vipya vimekuwa vikiongezeka.
Pili niwashukuru sana sana wabunge wote wawili wa majimbo ya Maswa, Maswa Mashariki chini ya Mhe, Stanislaus Nyongo (mb) ambaye pia ni naibu waziri wa madini ambapo kwa kila kata katika ka 19 zinazoounda jimbo hilo tumekuta vifaa vya michezo vimetolewa hasa mipira kila kijiji kwa kata zote 17 tumekuta hali ya kisiasa sio mbaya  Vijana na wanchi wanaunga juhudi zinazofanywa na mheshimiwa Mbunge na chini ya uongozi wa mheshimiwa Rais Doctor Magufuli bila kusahaulika katika suala LA uwezeshwaji wa vijana kila kata kwenye vikundi vitano tumekuta vikundi 2  vilipatiwa mkopo2016_2017. Aidha nimshukuru sana sana mheshimiwa mbunge wa Maswa Magharibi Mhe Mashimba Mashauri Ndaki kwa  ufuatiliaji wake wa ukaribu juu ya maslahi ya Vijana na wanachi kwa ujumla amekuwa karibu sana na wanchi wake hasa katika usimamizi wa miradi ya maendeleo ya wanchi na katika vikundi vya Vijana kwa maeneo makubwa hasa kata tuliuofika tumekuta vikundi na vingine tayari viliwezeahwa kwa mwaka 2016_2017, aiza mipira na jezi kwa Vijana hasa tuliowafikia iliwafikia kwa mwaka 2016_2017.
Nikishukuru Chama cha mapinduzi CCM chini ya Ungozi wa Mzee, Enginer Ndushi, na secretariti ya halmashauri kuu ya CCM ya wilaya chini ya Katibu wa Chama comred Novelty Kibaji kama timu moja wanafanya Nazi kubwa na ya kujitolea kuhakikisha Chama na jumuia zake zimekuwa imara na zinafanya kazi zake kwa Uhuru na maelewano na kufikia hatya nzuri ya Mafanikio ya Chama na jumuia #Asanteni sana kwa umhimu umoja wa Vijana tuna kutakia kila LA kheri  comrede Omary Mtuwa(aliyekuwa Katibu wa Chama cha mapinduzi Maswa sasa yupo pwani) ulisimamia vyema uchaguzi ndani ya Chama  na uchaguzi mdogo wa udiwani Nyabubinza kwa kushirikiana vizuri na kamati yetu ya siasa UVCCM na secretarieti na wanachama wote na CCM ilieendelea kuheshimika na kuaminika MUNGU akubariki popote ulipo.

Tunawashukuru sana Madiwani wote amabao kwa utiari wenu mmekuwa mkishirikiana nasi na katika kutuchangia pale tunapokwaa kubwa zaidi mlipokubali kuwachangia Vijana wenu kanuni za UVCCM ili Vijana wenu waendelee kufanya vikao vyao kwa mjibu wa kanuni MUNGU awabariki, kama jumuia tutawapa ushikiano pia tupo tayari.
Asanteni saana Vijana wenzangu kwa dhama hii kubwa katika MAISHA yangu nawaaahidi Ofisi yangu kupitia kwa Katibu wangu wa Vijana wilaya tupo tayari kuwasikiliza na kuwasaidia kwa muda wote. Asanteni kwa kuwa nami karibu.
Mwisho nakushukuru sana Baba na Mama yangu na Ndugu zangu wote kwa ushauri na malezi. Asante Mzee Gembe Baba yaangu.
Asanteni wana Maswa wote na viongozi wenzangu wa Chama na jumuia ndani ya Maswa na nje ya mipaka. MUNGU AWE NANYI NYOTE
        
Masaga Paul.     Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Maswa 0758092500....Dodoma Maswa

Comments

Popular posts from this blog

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MADINI MHESHIMIWA NYONGO MKOANI IRINGA....

MWANAMALUNDI, MSUKUMA ALIYEMSHINDA MKOLONI