ASANTE RC MTAKA KWA UAMUZI MZURI WA KUSHUSHA BEI KWA WATEJA WASIO NA MITA ZA MAJI
MKUU WA MKOA WA SIMIYU ASHUSHA BEI YA MAJI MASWA.
Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Antony Mtaka ameiagiza Mamlaka ya Maji na usafi wa Mazingira mjini Maswa(Mauwasa) kushusha bei ya maji kwa wateja wao wasio na dira(Mita)kutoka sh 25600 hadi Sh 17600 kwa mwezi.
Uamuzi huo ameutoa leo ktk viwanja vya Madeco mjini Maswa alipofanya mkutano wa hadhara wa kusikiliza malalamiko ya wananchi juu ya kupanda bei hizo kutoka Sh 5600 hadi Sh 25,600 na utekelezaji huo unaanza mwezi huu.
Na Samuel Mwanga_Maswa
Comments
Post a Comment