TUSICHUKULIE POA CORONA INAZUILIKA
Ndugu wadau wanahabari, vijana wenzangu, wasomaji pamoja na wasikilizaji wetu Habari zenu Binafsi.
Nianze kwa kuwakumbusha na kuwafahamisha kuwa bado Duniani kote wanahangaika, kuzuia na kupambana na ugonjwa huu wa Corona. hata hapa Tanzania tayari tumekuwa tukipokea Taarifa na hali ya udhihiti wa ugonjwa huu wa Corona hata hivyo Niwaombe muendelee kufuaata maelekezo ya serikali ya namna ya kujikinga pamoja na kuzitekeleza kwa vitendo tahadhari zinazotolewa kupitia wizara ya afya na kamati iliyoundwa na waziri mkuu.
Ndugu wadau wa habari na Wana maswa mnaotumia mitandao kazaa ya kijamii whatsp, Instagram, Facebook na mingineneo zitumieni mitandao hizo kwa kuendele kuelimisha na kuikumbusha jamii na pia kuhamasisha usafi na uchukuaji wa tahadhari zinazotolewa na serikali kwani mitandao ya kijamii imekuwa ni chachu ya kupokea na kutoa Taarifa zinazojili tumieni muda wenu wa kukaa katika Magroup hayo kwa faida na kushusha hamasa hizo kwa familia zetu na jamii zetu zinazotuzunhuka. Ugonjwa huu wa Corona nao utapita yamepita magonjwa mengi Lakini serikali imekuwa ikichukua hatu na kwa hili la Corona imeshachukua hatua na suala la kuelimisha jamii si la wizara peke yake au wakuu wa mikioa na wilaya peke yao ni letu sote jambo la msingi ni hayo maelekezo ya serikali bila kuongeza chumvi ni kuyapeleka katika jamii zetu ama Taasisi zetu.
Mwisho Kama vijana wazalendo wa taifa hili tuweni wa kusemeana Mema sisi kwa sisi Kama vijana maaa kesho yangu na kesho yenu hatujui Nani atakuwa Nani na msaada kwa mwenzake tupendaneni tusemeaneni kwa wema na tuendelee kuiunga mkono serikali Chini ya uongozi imara na usioyumba wa Dr John Pombe Joseph Magufuli na kuchapa kazi tu.
Hapa kazi tu Asante kwa kunisoma.
Comments
Post a Comment