Posts

ASANTE RC MTAKA KWA UAMUZI MZURI WA KUSHUSHA BEI KWA WATEJA WASIO NA MITA ZA MAJI

MKUU WA MKOA WA SIMIYU ASHUSHA BEI YA MAJI MASWA. Mkuu wa mkoa wa Simiyu,Antony Mtaka ameiagiza Mamlaka ya Maji na usafi wa Mazingira mjini Maswa(Mauwasa) kushusha bei ya maji kwa wateja wao wasio na dira(Mita)kutoka sh 25600 hadi Sh 17600 kwa mwezi. Uamuzi huo ameutoa leo ktk viwanja vya Madeco mjini Maswa alipofanya mkutano wa hadhara wa kusikiliza malalamiko ya wananchi juu ya kupanda bei hizo kutoka Sh 5600 hadi Sh 25,600 na utekelezaji huo unaanza mwezi huu. Na Samuel Mwanga _ Maswa

POLENI SANA AMCOs Shinyanga Mwenge_Dakama Maswa kwa Ajari ya moto Kuunguliwa kwa pamba, lakini hakikisheni wanchi mnawalipa kama tu walikuwa wana madai yao.

Nianze kwa kutoa pole kwa Chama cha kushirikiana wilaya ya Maswa mkoa wa simiyu Hasa  vingozi wa amcos Kata ya Dakama kijiji cha Shinyanga mwenge kwa  ajari ya moto Iliyotokea na kusababisha Ghara la  kuhifadhia Pamba kuungua na kusababisha Hasara kwa Amcos ya takribani tan 120000 zilizowaka moto aidha nitoe pole kwa wananchi wa Shinyanga kwa kupoteza rasilimali hii adimu katika maghara lakini Viongozi wa Amcos Shinyanga Mwenge walipeni wanchi kama mliwakopa na mkapima Pamba yao kisha mkaiifadhi kwa kusubiri fedha na ili mwalipe,  kuungua moto maghara yenu ni sawa na ajari zingine lakini mkulima asihusike na Hasara hii kwani yeye   aliihifadhi vyema na akauza kwenu sasa hii ni  yenu viongozi wa AMCOS. Hatuhitaji kusikia wanchi hawajalipwa eti kwa kisingizi cha moto, moto ni  ajari kwenu na Hasara yenu kama Chama cha ushirika. Aidha niwaombe wanchi na vijana wenzetu muwe watulivu na wavumulivu na kuyafuata Yale viongozi wa cham cha ushirika na ser...

MJUE BIBI TITI MWANAMKE SHUJAA NA HODARI MWENYE HISTORIA YA KPKEE TANZANIA

+255 🇹🇿🇹🇿🇹🇿 BIBI TITI MOHAMED: MWANAMAMA SHUPAVU NA MPIGANIA UHURU HODARI ALIYETINGISHA NA KUHESHIMIKA AFRIKA MASHARIKI NZIMA!!! 1. Usuli: 1.1 TITI Kuzaliwa: TITI MOHAMED SALUM MANDWAGA alizaliwa mwezi Juni 1926 jijini Dsm. 1.2 Wazazi Wa TITI: Baba yake aliitwa Bw. MOHAMED BIN SALIM na mama yake aliitwa Bi. HADIJA BINTI SALIM. Wazazi hawa walitokea Rufiji. Baba yake alikuwa mfanyabiashara ya mbuzi na ng'ombe na mama yake alikuwa mkulima. 2. Elimu: 2.1 Baba Agoma TITI Asisome: Baba yake alikataa katukatu kwamba TITI asisome shule kwa hofu angekuwa kafiri. 2.2 Mama Ampeleka TITI Shule: Baba yake alifariki TITI akiwa na miaka 9 tu. Mamaye akatumia fursa hiyo kumpeleka TITI Shule ya Wasichana Uhuru ambako alisoma hadi darasa la 4. 3. TITI Aolewa na MHENGA akiwa na miaka 14 tu: TITI aliolewa na mwanaume mzee ambaye angeweza hata kuwa baba yake wakati yeye akiwa binti wa miaka 14 tu. 4. TITI Ajifungua M...

ZIARA YA NAIBU WAZIRI WA MADINI MHESHIMIWA NYONGO MKOANI IRINGA....

Image
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo leo Januari 14, ameanza rasmi ziara ya kukagua shughuli za uchimbaji madini katika Mkoa wa Iringa. Akiwa Mkoani humo, Naibu Waziri ametembelea  na kukagua mgodi wa Ulata katika kijiji cha Ulata, Kata ya Uwasa Wilaya ya Iringa. Mbali ya kutembelea mgodi huo, pia amesikiliza kero za wachimbaji mgodi hapo akilenga kutatua mgogoro  baina ya mmiliki wa mgodi huo na wachimbaji wadogo. Aidha, mbali ya kutatua mgogoro huo, amepata fursa ya kuzungumza na wachimbaji hao  ambao wametoa kero zao. Taarifa zaidi kuhusu alichokizungumza Naibu Waziri itawaijia. Tangaza Nasi UVCCM Maswa  Bureee kupitia Blog   yetu Tushirikishe 0758092500

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CCM MASWA MKOANI SIMIYU YALETA NEEMA UKAMILISHWAJI WA JENGO LA KITEGA UCHUMI LA CCM. NYONGO ASHITUKIZA HARAMBEE

Image
Ziara ya katibu mkuu wa  chama cha mapinduzi CCM Taifa  Dr Bashiru Ally mkoani Simiyu Imetamatika katika wilaya ya Maswa ambapo pamoja na Mambo mengine Dr. Bashiru Ally aliweza kusimika Jiwe la  Msingi la  ujenzi wa  jengo la  kitega uchumi. na kuwahutubia mamia ya wanachama wa  CCM waliojitokeza kwa wingi kumraki na kumsikiliza katibu mkuu wa   CCM . katika hatua nyingine Mbunge wa Maswa  Mashariki na Naibu waziri wa  Madini Mheshimiwa Stanslaus . H. Nyongo alipopata wasaa wa  kusalimia aliweza kuhamasisha Harambee ya Papo kwa hapo   ili kukamilisha baazi ya mahitaji ya Jengo hilo Ambapo Mheshimiwa nyongo akiwa kama katibu wa  wabunge wa mkoa wa  simiyu aliwaita wabunge wote   waliokuwepo na akawaomba wamchangie chochote kwaajili ya ukamilishaji waa jengo hilo . Mhe   Nyongo alitoa mifuko 100 ya cement, na wabunge wote   walichangia Bati 150  wak...

KUTOKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MWALIMU JULIUS NYERERE DAR.

Image
YALIYOJIRI WAKATI WA MAPOKEZI YA NDEGE MPYA YA AIRBUS 220-300 KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE LEO TAREHE 23 DESEMBA, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli #Nawapongeza watanzania kwa kuamua kulipa kodi, tunafanya haya kwa sababu ya kulipa kodi, hongereni sana Watanzania. #Watanzania nawasisitiza tuwe wazalendo, hii ni kwa faida ya taifa letu. #Uchumi wa nchi yetu unaenda vizuri, tutunze amani yetu, tunarasilimali nyingi, Tanzania ni tajiri. #Pamoja na kuleta ndege mpya tunafufua karakana yetu kubwa ya matengenezo ya ndege iliyopo Kilimanjaro. #Tuliahidi kuimarisha huduma za usafiri, na katika miaka hii mitatu tumetekeleza ahadi hii kwa vitendo ikiwa ni kwa kufanya mambo makubwa ardhini, angani na hata majini. #Tunafanya upanuzi na ukarabati wa viwanja vya ndege 11 nchini, lengo ni kuendelea kuboresha sekta ya usafiri  wa anga. #Watendaji wakuu wa Serikali waliolipiwa tiketi za ndege za ATCL na hawakusafiri warudishe fedh...

MWANAMALUNDI, MSUKUMA ALIYEMSHINDA MKOLONI

Image
Kwa Hisani ya Mwandishi wa  kitabu chake NG'WANAMALUNDI SHUJAA WA WAKISUKUMA ALIYEWATESA WAJERUMANI. Kwa wale waliopata kusoma historia au kusikia hadithi za makabila, hasa ya Wasukuma na Wanyamwezi, hawakukosa kusikia habari ya Ng’wanamalundi. Mtu huyo aliyewahi kuutingisha utawala wa Wajerumani, alizaliwa katika ukoo wa kawaida akiwa mcheza ngoma mashuhuri, mwaka wa kuzaliwa kwake haufahamiki ila alifariki dunia mwaka 1936, akiwa tayari mtu mzima. Watu wengi wamekuwa wakimjadili kwa maoni tofauti, wengine wakimsifu kama shujaa huku wengine wakihusisha uwezo wake na nguvu za giza. Katika makala hii usahihi wa historia yake unaelezwa na mjukuu wake wa pili, Kishosha Sitta (80) mkazi wa Kijiji cha Mwalugulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, anayesimulia alivyomfahamu babu yake huyo. Sitta anaanza kueleza kuwa jina halisi la babu yake halikuwa Ng’wanamalundi bali lilikuwa Igulu Bugomola, ambaye alizaliwa katika Kijiji cha Mwakubunga Nera wilayani Kwimba mkoani Mwa...