Posts

KUTOKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MWALIMU JULIUS NYERERE DAR.

Image
YALIYOJIRI WAKATI WA MAPOKEZI YA NDEGE MPYA YA AIRBUS 220-300 KATIKA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE LEO TAREHE 23 DESEMBA, 2018 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli #Nawapongeza watanzania kwa kuamua kulipa kodi, tunafanya haya kwa sababu ya kulipa kodi, hongereni sana Watanzania. #Watanzania nawasisitiza tuwe wazalendo, hii ni kwa faida ya taifa letu. #Uchumi wa nchi yetu unaenda vizuri, tutunze amani yetu, tunarasilimali nyingi, Tanzania ni tajiri. #Pamoja na kuleta ndege mpya tunafufua karakana yetu kubwa ya matengenezo ya ndege iliyopo Kilimanjaro. #Tuliahidi kuimarisha huduma za usafiri, na katika miaka hii mitatu tumetekeleza ahadi hii kwa vitendo ikiwa ni kwa kufanya mambo makubwa ardhini, angani na hata majini. #Tunafanya upanuzi na ukarabati wa viwanja vya ndege 11 nchini, lengo ni kuendelea kuboresha sekta ya usafiri  wa anga. #Watendaji wakuu wa Serikali waliolipiwa tiketi za ndege za ATCL na hawakusafiri warudishe fedh...

MWANAMALUNDI, MSUKUMA ALIYEMSHINDA MKOLONI

Image
Kwa Hisani ya Mwandishi wa  kitabu chake NG'WANAMALUNDI SHUJAA WA WAKISUKUMA ALIYEWATESA WAJERUMANI. Kwa wale waliopata kusoma historia au kusikia hadithi za makabila, hasa ya Wasukuma na Wanyamwezi, hawakukosa kusikia habari ya Ng’wanamalundi. Mtu huyo aliyewahi kuutingisha utawala wa Wajerumani, alizaliwa katika ukoo wa kawaida akiwa mcheza ngoma mashuhuri, mwaka wa kuzaliwa kwake haufahamiki ila alifariki dunia mwaka 1936, akiwa tayari mtu mzima. Watu wengi wamekuwa wakimjadili kwa maoni tofauti, wengine wakimsifu kama shujaa huku wengine wakihusisha uwezo wake na nguvu za giza. Katika makala hii usahihi wa historia yake unaelezwa na mjukuu wake wa pili, Kishosha Sitta (80) mkazi wa Kijiji cha Mwalugulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga, anayesimulia alivyomfahamu babu yake huyo. Sitta anaanza kueleza kuwa jina halisi la babu yake halikuwa Ng’wanamalundi bali lilikuwa Igulu Bugomola, ambaye alizaliwa katika Kijiji cha Mwakubunga Nera wilayani Kwimba mkoani Mwa...

Mwaka mmoja wa Mwenyekiti wa UVCCM (w) maswa.

Image
Ni mwaka mmoja sasa tangu uchaguzi wa Chama NA jumuia Ngazi ya wilaya NA kukamilika kwa safu ya uongozi kwa ngazi ya wilaya NA jumuia zake, Naam nilipata dhamana kubwa ya kuiongoza jumuia ya Vijana wenzangu kwa ngazi ya wilaya nikipata heshima ya kuwa Mwenyekiti uchaguzi uliokuwa wa Uhuru NA haki. Jumuia ya Vijana ni jumuia ambayo imebeba Leo yao NA kesho yao kwa vijana tunajitahidi sana kuyasemea mahitaji yao. NA pia kuzitatua changamoto zao kazaa, ikiwemo Ajira, Elimu, ujasiriamali, Mikopo vyuo na vyuo vikuu uwezeshwaji wa vijana hasa kupitia miradi yao kama MBOs, NGs, na hasa uwezeshwaji wao wa mikopo nafuu Kutoka halmashauri yetu ya Maswa. Lakini katika kipindi hiki cha mwaka mmoja tumeendelea kuwafikia vijana wenzetu hasa kupitia ziara ambapo tunapata nafasi ya kuwasikiliza kuwashauri na kuwajengea uwezo na kuwapa Hamasa ya kuyakabiri MAISHA ndani ya Chama na MAISHA ya kawaida nje ya Chama ( we are  empowering them and sensitizes, for their self awareness) ili kupata vijana s...

KUELEKEA MTIHANI WA TAIFA MWEZI MEI, WANAFUNZI 1003 KIDATO CHA SITA SIMIYU WAPIGA KAMBI YA KITAALUMA

Na Stella Kalinga Simiyu Takribani wanafunzi 1003 wa Kidato cha sita kutoka shule za Sekondri 11 zenye kidato cha tano na sita Mkoani Simiyu wamepiga kambi katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa na Shule ya Sekondari Binza, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Mtihani wa Taifa ambao unatarajia kufanyika mapema mwezi Mei mwaka huu. Akifungua kambi hiyo leo  katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Maswa wilayani Maswa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe.Anthony Mtaka amesema ili mkoa huo uweze kushindana na kufanya mageuzi katika Uchumi ni lazima kuwekeza katika elimu. “Kama wanafunzi wetu wanakaa makambi ya michezo ngazi ya kata, wilaya, mkoa na Taifa kwa nini wanafunzi hao hao wasikae  kambi kwa ajili ya maendeleo ya taaluma; tukitaka kufanya mageuzi ya Mkoa huu ni lazima tuweke nguvu kwenye elimu, maeneo yenye uchumi mzuri wamewekeza sana kwenye elimu” alisema Mtaka. Aidha, Mtaka awataka wanafunzi wote wa kidato cha sita kuwasikiliza walimu watakaokuwa wakiwafu...

TUUNGE MKONO JUHUDI ZA VIONGOZI WETU TUIJENGE MASWA YETU

Image
      MASWA YETU          Anaandika mothes mbembela Ndugu wapenzi wasomaji wa Makala zangu Napenda kuwaalika tena katika uchambuzi wa makala zangu ambazo mara nyingi zimekuwa zikiegemea katika kujadili masuala mbalimbali kutoka katika wilaya yangu ya Maswa mkoani Simiyu. Leo katika makala hii ningependa kujikita zaidi katika kutabainisha mambo mbalimbali ya kijamii, kiuchumi na kisiasa ambayo kwa kiasi kikubwa yanafanya MASWA YETU ionekane angavu Daima. Katika wilaya yetu Maswa Juhudi mbalimbali zimeweza kufanywa na viongozi kwa kushirikiana na wananchi wao kuhakikisha kuwa wilaya yetu haipo mbali ktk kilele cha maendeleo, kwa ufupi tu niweze kuorodhesha mambo na assets mbalimbali ambazo kwa Hakika Maswa Tunajivunia. 1. Tuna Hospitali kubwa ya wilaya ambayo imekuwa ikihudumia maelfu ya wagonjwa kutoka sehem mbalimbali za nchi yetu tena kwa kiwango cha juu kabisa (Science and Technology) Hongera ya pekee imfikie Dokta...

MAANDAMANO YA CHADEMA KUPITIA KWA MANGE KUNAMBI NI HARAMU WASHIRIKI KUKIONA CHA MTEMAKUNI

Na David Maphone. . NI KWA MUJIBU WA SHERIA NA KATIBA YA  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA , . . Ni vyema tujaribu kuangalia  ni nani anaitisha MAANDAMANO nini kilichoombwa katika hayo MAANDAMANO na nini  kilichozuiwa na POLISI katika hayo MAANDAMANO ?. Pia kuangalia sheria inasemaje kuhusu suala hili. NINI  HAKI AU STAHILI (ENTITLEMENTS) ZA VYAMA VYA SIASA KUHUSU  MAANDAMANO NA MIKUTANO ?: #Sheria za Vyama vya Siasa (Political Parties Act) na za Jeshi la Polisi (Police Force and Auxiliary Services Act) zinatoa stahili ya kufanya mikutano ya hadhara (Public Meetings) na kuongozana (Processions) kwa vyama vya Siasa kwa ajili ya kujitangaza na kutafuta wanachama,  Kifungu cha (4) cha sheria ya vyama kinatoa haki hiyo Lakini Kifungu cha (6) cha sheria hiyo hiyo kinatoa Sharti ili chama kifanye maandamano au mkutano wa Hadhara.'' Chama hakitaruhusiwa kufanya mkutano au Maandamano kama kitapokea AMRI PINGAMIZI kutoka Jeshi la POLISI''. #Pia sheria inatoa ...

TUONGEZE JUHUDI KUFANYA KAZI NA KUMPA USHIRIKIANO RAIS WETU

Image
Nianze kwa kuwapa pole na majukumu mazito kwenu viongozi na watanzania wote popote mlipo kwa kazi na majukum makubwa ya kila siku mnayofanya, hii yote ni katika kuutengeneza mkate wa kila siku na wajibu wako kama sehemu ya kuijenga Tanzania mpya na familia zetu. Sambamba na pole hii niwapongeze kwa kazi nzuri mnazozifanya kuhakikisha tanzania yetu inasonga mbele (SISI NI TANZANIA MPYA). hakuna asiyejua kuwa zama hizi ni zama za kazi na hasa kazi ya kuijenga Tanzania mpya Tanzania ya uchumi wa kati na ya viwanda naomba kusema yafuatayo. ndugu watanzaia wenzangu Tanzania mpya ni Tanzania ambayo watu wake wanapaswa kuwa wazalendo  katika kutimiza majuku yetu ya kila siku kwa nafasi zetu tofauti tofauti ni wajibu wetu kufanya kazi kizalendo ili kutimiza wajibu wetu vizuri wa kuijenga Tanzania mya.  Tanzania tunayo bahati kubwa kuwa miongoni mwa taifa ambalo Rais wake ni Mzalendo anayelipenda taifa lake kwa moyo wake wote na nguvu zake zote zote, anfanya kazi kubwa yeye pa...