Ndugu wadau wanahabari, vijana wenzangu, wasomaji pamoja na wasikilizaji wetu Habari zenu Binafsi. Nianze kwa kuwakumbusha na kuwafahamisha kuwa bado Duniani kote wanahangaika, kuzuia na kupambana na ugonjwa huu wa Corona. hata hapa Tanzania tayari tumekuwa tukipokea Taarifa na hali ya udhihiti wa ugonjwa huu wa Corona hata hivyo Niwaombe muendelee kufuaata maelekezo ya serikali ya namna ya kujikinga pamoja na kuzitekeleza kwa vitendo tahadhari zinazotolewa kupitia wizara ya afya na kamati iliyoundwa na waziri mkuu. Ndugu wadau wa habari na Wana maswa mnaotumia mitandao kazaa ya kijamii whatsp, Instagram, Facebook na mingineneo zitumieni mitandao hizo kwa kuendele kuelimisha na kuikumbusha jamii na pia kuhamasisha usafi na uchukuaji wa tahadhari zinazotolewa na serikali kwani mitandao ya kijamii imekuwa ni chachu ya kupokea na kutoa Taarifa zinazojili tumieni muda wenu wa kukaa katika Magroup hayo kwa faida na kushusha hamasa hizo kwa familia zetu na jamii zetu zinazotuzunhuka. Ug...