Posts

Mti mwema. Wenye maajabu.

Basi kukapambazuka siku yenyewe na mvua ilikuwa Bado inanyesha hata hivyo ilikuwa mvua ya wastani japokuwa watu hawakukata tamaa kuelekea kunako shughuli zao za Kila siku. Wakati tunatoka Ndani ya nyumba nje yake kulikuwa na mti aina ya mkwaju nikashangaa kuona matunda yake yakiwa yamekomaa yamewiva vizuri lakini matunda menyewe yapo utupu yaani yamemenywa ingali Bado yapo mtini na Kwa sababu ya mvua na unyevu ukwaju ule ulikuwa ukinata, Cha ajabu nilipotaka kuchuma walau tunda mojawapo ndipo macho yangu yakakutana uso Kwa uso na joka kubwa aina ya chatu, Ambapo kwenye huo mti lipo pango joka Hilo linaishi. Joka Hilo kubwa likaanza kutuvizia kuja upande tuliokuwa  kutaka kutumeza hata hivyo mawe yaliyokuwa chini, ng'hambo kidogo tuliyatumia kuliponda na baadae likawa limerudi Ndani ya pango lake kwenye utando wa mti huo wa mkwaju. Nikamwambia rafiki yangu mti huu hupondwa si Kwa sababu ya matunda Ila hupondwa Kwa sababu joka hili  juu ya mti, katikati linaziba au kuzuia ridhiki ya ...

SIMANZI

UVCCM Maswa tumepokea Taarifa ya simanzi ya ajari Mbaya  ya gari iliyokuwa katika msafara wa mkuu wa mkoa Mwanza wakitokea ukelewe kupitia bunda ambapo wakiwa Busega gari iliyokuwa na waandishi wa Habari kugongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya Raia 14 wakiwemo wandishi kazaa. Roho za Marehemu zipumuzike kwa amani.       Masaga Paul Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Maswa.

KHERI YA MWAKA MPYA

Kwaniaba ya Umoja wa vijana wa chama Cha mapinduzi Wilaya ya Maswa, napenda kuwatakia Kheri ya mwaka mpya 2022. Ukawe mwaka wenye Kheri ,neema na Mafanikio makubwa kwa kila mmoja wetu. Masaga John Paul. Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Maswa (M/k/ siasa)

SAMIA TENA 2025-30

Kwa Niaba ya vijana wote Kanda ya ziwa na  Kati bila ya kujari itikadi zetu za Dini ,siasa, ukanda au vyama vyetu vya siasa. Tunakupongeza kwa kuendeleza vyema taifa letu Tanzania kwa kudumisha Amani, Mshikamano na ustawi wa jamii. Taifa linasonga mbele kisiasa, uchumi na hata kijamii. Hongera Mhe SAMIA SULUHU HASSAN Vijana tunakuelewa zaidi.

TUMEWAKOSEA WAMACHINGA

* Msimamo wangu Binafsi juu ya suala la Machinga * Kwanza nitoe pole kwa ghasia na taharuki na Mabadiriko ya ghafla zidi ya waMachinga Bodaboda, Mama Rishe na woote walioghubikwa na Mambo ya kupangana mjini na huenda vijijini. Kwangu Binafsi naona mmewakosea Sana kundi la jamii hii ya wafanya kazi na haswaa waliojiajiri kupitia umachinga. Na Declare intest kuwa Mimi Ni Machinga. Pia nakubaliana na Mpango mzuri wa serikali kwa tunachokiita Uwepo wa mpango wa maeneo maalum ya biashara za wamachinga na namna Boda boda watakavyokuwa wanaingia na kutoka mjini. Lakini wateule mmekurupupa mno juu ya Jambo hili na mmegharimu maisha yetu na Maisha ya wanchi (siwaiti wanyonge nawaita wajenzi wa taifa na walipa Kodi). Suala hili lilipaswa liwe shirikishi na Mpango wa muda mrefu wa kubainisha maeneo, changamoto  zao  na utaratibu mzuri wa kazi zao za  kichinga na Bodaboda kabla ya kutufurumusha,  sio suala la kukurupushana namna hiii (Chama changu kupitia mwenenezi taifa nakubaliana na kauli ku...

DAKIKA 45 ZA KIPINDI CHA KWANZA KWANU WATEULE

Image
  Ndugu watanzania wenzangu , mabibi na mabwana vijana kwa wazee, nianze kwa kumshukuru Mungu kwa uzima na afya njema kwetu sote lakini nitoe pole kwa wale wote ambao hali zenu sio nzuri kiafya pamoja na mambo mengine, hata hivyo kila lililo kheri nawatakieni. Nianze kwa kumpongeza Dr John Pombe Magufuli Rais wa awamu ya tano wa jamhuri ya muungano wa Tanzania  kwa mara nyingine kwa  kuaminiwa na watanzania wote kuendelea kuwaongoza kwa ushindi wa kishindo wa zaidi ya asilimia 81, wakiwa pamoja na mwana mama hodari kabisa Samia Hassan katika uchaguzi mkuu wa october 2020. lakini kwa kipekee nikipongeze chama cha mapinduzi CCM chini ya uongozi wa dr John Pombe Magufuli kwa kuendelea kuaminika na Umma wa Tanzania  hata hivyo pongezi ziende kwao viongozi wa CCM wa ngazi zote kwa kazi kubwa walizofanya katika kuhakikisha CCM inaendelea kushinda chaguzi ili kuunda serikali. niishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kutekeleza vyema na kishindo ilani ya uchaguzi ya mwaka 20...

TUSICHUKULIE POA CORONA INAZUILIKA

Image
Ndugu wadau wanahabari, vijana wenzangu, wasomaji pamoja na wasikilizaji wetu Habari zenu Binafsi. Nianze kwa kuwakumbusha na kuwafahamisha kuwa bado Duniani kote wanahangaika, kuzuia na kupambana na ugonjwa huu wa Corona. hata hapa Tanzania tayari tumekuwa tukipokea Taarifa na hali ya udhihiti wa ugonjwa huu wa Corona hata hivyo Niwaombe muendelee kufuaata maelekezo ya serikali ya namna ya kujikinga pamoja na kuzitekeleza kwa vitendo tahadhari zinazotolewa kupitia wizara ya afya na kamati iliyoundwa na waziri mkuu. Ndugu wadau wa habari  na Wana maswa mnaotumia mitandao kazaa ya kijamii whatsp, Instagram, Facebook na mingineneo zitumieni mitandao hizo kwa kuendele kuelimisha na kuikumbusha jamii na pia kuhamasisha usafi na uchukuaji wa tahadhari zinazotolewa na serikali kwani mitandao ya kijamii imekuwa ni chachu ya kupokea na kutoa Taarifa zinazojili tumieni muda wenu wa kukaa katika Magroup hayo kwa faida na kushusha hamasa hizo kwa familia zetu na jamii zetu zinazotuzunhuka. Ug...