Posts

ASANTENI WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA CCM WILAYA YA MASWA

Mmenipa dhamana Ambayo kwangu naiona ni Bahati nzuri nitaitenda kama mlivyonituma Nitalipa wema Kwa wote  *Hodi mkoani tena

MUDA WA KUHESABIWA UMEWADIA HIVI SASA

Ndugu wananchi wenzangu,  Muda umeshawadia wa serikali yako kupata taarifa ya idadi yenu katika nzengo yenu hakikisha umehesabiwa hii ni Mhimu kwako, nzengo yako na serikali yako JITOKEZE UHESABIWE.

KUHESABIWA NI KUISAIDIA SERIKALI YAKO Ili IKUFIKIE

Kila mmoja ajiandae Kwa kuhesabiwa kwa kutoa taarifa sahihi za kidemographia na uchumi ili Taifa letu lipange na kuwa na mpango sahihi wa utekelezaji sahihi wa maendeleo ya Taifa letu kwa kufuata mlinganyo sahihi wa idadi sahihi ya watu na mpangilio sahihi wa makazi yetu SERIKALI NI KAMA FAMILIA lazima ujue idadi na mahitaji sahihi Kwa Wana familia. Usiku wa kuamkia 23/08/2022 kuwa tayali kuhesabiwa Onyesha ushirikiano Kwa makarani wa sensa. MASAGA JOHN PAUL     Mwasiliwa wa kutokuwa na idadi kamili ya Wana nzengo katika Kijiji CHANGU  maendeleo tunayapata Kwa kukadiliwa idadi yetu Jitokeze uhesabiwe

Mti mwema. Wenye maajabu.

Basi kukapambazuka siku yenyewe na mvua ilikuwa Bado inanyesha hata hivyo ilikuwa mvua ya wastani japokuwa watu hawakukata tamaa kuelekea kunako shughuli zao za Kila siku. Wakati tunatoka Ndani ya nyumba nje yake kulikuwa na mti aina ya mkwaju nikashangaa kuona matunda yake yakiwa yamekomaa yamewiva vizuri lakini matunda menyewe yapo utupu yaani yamemenywa ingali Bado yapo mtini na Kwa sababu ya mvua na unyevu ukwaju ule ulikuwa ukinata, Cha ajabu nilipotaka kuchuma walau tunda mojawapo ndipo macho yangu yakakutana uso Kwa uso na joka kubwa aina ya chatu, Ambapo kwenye huo mti lipo pango joka Hilo linaishi. Joka Hilo kubwa likaanza kutuvizia kuja upande tuliokuwa  kutaka kutumeza hata hivyo mawe yaliyokuwa chini, ng'hambo kidogo tuliyatumia kuliponda na baadae likawa limerudi Ndani ya pango lake kwenye utando wa mti huo wa mkwaju. Nikamwambia rafiki yangu mti huu hupondwa si Kwa sababu ya matunda Ila hupondwa Kwa sababu joka hili  juu ya mti, katikati linaziba au kuzuia ridhiki ya ...

SIMANZI

UVCCM Maswa tumepokea Taarifa ya simanzi ya ajari Mbaya  ya gari iliyokuwa katika msafara wa mkuu wa mkoa Mwanza wakitokea ukelewe kupitia bunda ambapo wakiwa Busega gari iliyokuwa na waandishi wa Habari kugongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya Raia 14 wakiwemo wandishi kazaa. Roho za Marehemu zipumuzike kwa amani.       Masaga Paul Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Maswa.

KHERI YA MWAKA MPYA

Kwaniaba ya Umoja wa vijana wa chama Cha mapinduzi Wilaya ya Maswa, napenda kuwatakia Kheri ya mwaka mpya 2022. Ukawe mwaka wenye Kheri ,neema na Mafanikio makubwa kwa kila mmoja wetu. Masaga John Paul. Mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Maswa (M/k/ siasa)

SAMIA TENA 2025-30

Kwa Niaba ya vijana wote Kanda ya ziwa na  Kati bila ya kujari itikadi zetu za Dini ,siasa, ukanda au vyama vyetu vya siasa. Tunakupongeza kwa kuendeleza vyema taifa letu Tanzania kwa kudumisha Amani, Mshikamano na ustawi wa jamii. Taifa linasonga mbele kisiasa, uchumi na hata kijamii. Hongera Mhe SAMIA SULUHU HASSAN Vijana tunakuelewa zaidi.